Maelezo ya kidahizo

 

Kidahizo cha Kikabwa kwenye kamusi kinaonyesha neno la Kikabwa, ambalo ni kiunga, likifuatwa na kifupisho kwa aina yake ya usemi.  Ndipo tafsiri zinafuata kuanzia na Kiswahili na kumalizia na Kiingereza. Tafsiri hizi zinaweza kufuatwa na sentensi ya mfano na viunga vya vidahizo vinavyohusiana.

 

bhoono ke sasa; now

 

*eginguru nm nguvu; power, strength; Hanu ritariho ering'ana rya Waryubha, eginguru gya Erisambwa giraamba okutunga.Pasipo neno la Mungu, nguvu za Shetani zinaanza kutawala.; Where the word of God doesn't exist, the power of Satan begins to rule.

Kidahizo chenye zaidi ya maana moja kinorodhesha maana hizo baada ya kila namba.

 

*ahasi nm 1) mahali, sehemu; location, place

2) eneo; area