Wakabwa wanathamini sana lugha yao, ambayo inatumika nyumbani na kwa mikutano ya kijamii. Jitihada za kuendeleza lugha yao zimezalisha mfumo wa kuandika, maandiko mbalimbali, mafunzo ya kisomi na maendeleo ya kamusi. Idadi ya Wakabwa ambao wanaweza kusoma na kuandika lugha yao ni ndogo, lakini imeanza kukua. Mnamo 75% ya Wakabwa wanaweza kusoma na kuandika katika Kiswahili, ambacho ni lugha inayotumika sana maeneo yote ya Tanzania.
Kikabwa kimeanza kuchunguzwa na wanaisimu (linguists) tangu mwaka wa 2006. Kati ya mwaka wa 2009 na mwaka huu, maandiko mengine yamechapishwa, zikiwemo sehemu za Biblia.